Madaktari Bingwa wa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Aprili 07 ,2024 wameanza kufanya kazi za kitabibu katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Njombe (Kibena )
Akizungumza Dkt. Elestina Mwipopo Daktari wa Watoto ambaye ni mkuu wa msafara wa madaktari bingwa waliopo Halmashauri ya mji Njombe katika Hospitali ya kibena amesema kuwa tayari huduma zimeanza kutolewa kwa watoto,kinamama pamoja na kuwaona wagojwa ambao wametoka maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya mji Njombe.
Daktari Mwipopo amewaombwa wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kupata hudumu za kibingwa ili kupunguza gharama za matumizi makubwa ya fedha za kwenda maeneo mengine nje ya mkoa wa Njombe.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya kibena Daktari Ayoub Mtulo amesema wagonjwa wanafika kwa wingi kupata matibabu ya uzazi ,watoto na magonjwa ya ndani .
Nao baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kupata matibabu kwa madktari bingwa akiwemo Grace Fungo amesema anaishukuru Serikali kwa kuwaleta madktari bingwa ambao watamsaidia kutatua changamoto ya moyo kwa mtoto wake.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe