Idara ya Maendeleo ya Jamii ya Halmashauri ya Mji Njombe kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Boimanda imefanya shughuli za uchimbaji wa mawe na kusoma kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya mtendaji kijiji cha Boimanda kwa lengo la kuhamasisha moyo wa kujitolea na kushiriki katika maendeleo ya kijiji chao.
Akizungumza oktoba 06, 2025 mara baada ya zoezi Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Bi. Enembora Lema, amesema kuwa lengo kuu la tukio hilo ni kuimarisha mshikamano na kuwajengea wananchi moyo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.
“Tumekuja hapa leo sio tu kwa ajili ya kufanya kazi za kijamii, bali pia kuwatia moyo wananchi wetu kwamba maendeleo ya kweli huanzia na sisi wenyewe,Tunahitaji kushirikiana, kujitolea, na kuamini katika mabadiliko tunayoyatamani,” alisema Bi. Lema Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii
Katika zoezi hilo, maafisa kutoka idara hiyo walitoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala migogoro ya ardhi,ndoa na mirathipamoja na malezi bora ya watoto katika familia
Nao wanachi walioshiriki zoezi hilo akiwemo Beno Mgaya , James Mwajombe Wananchi na Sebastiani Mgaya walioshiriki walionesha furaha na kuthamini juhudi hizo, wakisema kuwa elimu waliyopewa ni muhimu sana katika kuimarisha ustawi wa familia na kijiji kwa ujumla huku wakisema jitihada hizo zimewapa motisha ya kuendelea kushiriki katika shughuli za kijamii na kuhamasisha wengine kufanya hivyo .
Zoezi hilo limekuwa likileta matokeo chanya kwa maeneo ambayo idara ya maendeleo ya jamii wamekuwa wakipitia vijiji vingine vya halmashauri hiyo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe