Serikali imechukua hatua za makusudi kuhakikisha pembejeo za kilimo zinapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu.
Pia Serikali inaendelea kuboresha miundombinu kwenye sekta ya umwagiliaji , ujenzi wa majosho na kutoa ruzuku ya dawa za kuogesha mifugo,uboreshaji wa miundombinu ya barabara kuanzia maeneo ya uzalishaji hadi sokoni pamoja nakuendelea na programu ya BBT yakuwasaidia vijana Kujenga Kesho iliyo Bora kupitia kilimo.
Wakati Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ikiendelea kufanya haya yote, Elimu ,ujuzi na Maarifa ni muhimu kwako mdau wa sekta ya Kilimo, mifugo na Uvuvi na hii ndiyo maana ya uwepo wa maonesho haya ya wakulima.
Hakikisha unazitumia vizuri siku nane kupata maarifa mapya kutoka kwa wataalamu na wakulima wazoefu watakaokuwepo kwenye banda la Halmashauri ya Mji Njombe katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Usikubali kulima wala kufuga kwa mazoea.Mali ipo shambani ,Lima na fanya ufugaji kwa tija.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe