• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Jafo afurahishwa na miradi ya kimkakati Halmashauri ya Mji Njombe,Wakandarasi walia na msamaha wa VAT

Tarehe iliyowekwa: May 31st, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za   Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo ameonyesha kufurahishwa na ujenzi wa soko la kisasa katika Halmashauri ya Mji Njombe ujenzi ambao unatarajiwa kukamilika ifikapo octoba 2019 na kugharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 9.1

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kuona shughuli za ujenzi zinazoendelea katika soko hilo Jafo amesema kuwa licha ya kuwepo na ujenzi wa miradi ya masoko katika Mikoa ya Mtwara, Dodoma, Morogoro na Dar es Salaam   ujenzi wa soko la Njombe ni wa kipekee na wenye viwango vya hali ya juu na kufurahishwa na namna Halmashauri ilivyoweza kuwashirikisha wafanyabiashara katika kila hatua za ujenzi na kutoa ushauri wao na kwa jinsi Halmashauri ilivyoweza kubuni na kutenga eneo kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua ambayo yatakuwa yakihudumia eneo lote la soko  jambo ambalo limekuwa halitekelezwi kwenye miradi mingi.

“Mimi huwa nakuja kukagua kazi sio kutembelea. Binafsi nimeridhishwa na kufurahishwa sana na ujenzi unaoendelea wa soko. Hiki ni kitega uchumi kikubwa sana kwa Halmashauri na kitabadili mandhari ya Mji wa Njombe. Katika Kanda ya Nyanda za juu kusini soko hili litakuwa la kipekee niwapongeze mmefanya kazi nzuri na hamjanitia hasira. Mkandarasi unafanya kazi nzuri sana na ninaomba uhakikishe kuwa unamaliza kazi kwa wakati.”Alisema Jafo.

Awali akipokea taarifa ya maendeleo ya shughuli za uendeshaji wa stendi na umaliziaji wa ujenzi kutoka kwa Mratibu wa Mradi Mhandisi Damasco Tembo, Mhandisi huyo alisema kuwa kwa sasa ujenzi wa stendi hiyo   umekamilika kwa asilimia 96 na unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Juni 2019  na kubainisha changamoto kubwa ya kutopatiwa kwa  msamaha wa ongezeko la thamani VAT kwa Wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa mradi wa soko na stendi jambo linakwamisha kukamilika kwa wakati kwa miradi hiyo.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa hiyo Jafo ameahidi kushughulikia changamoto ya msamaha wa ongezeko la thamani VAT changamoto iliyoibuliwa na wakandarasi wote wanaotekeleza ujenzi wa mradi wa soko na stendi na ameitaka Halmashauri kupata suluhu ya jambo lililokwamisha uwepo wa ujenzi wa kituo cha mafuta ndani ya stendi kama ilivyokuwa kwenye mchoro wa awali.

“Lengo la miradi hii ni kwa ajili ya kukuza Miji na kuzijengea Halmashauri uwezo wa kujitegemea. Kama ramani ya stendi hii ilikua na eneo la kituo cha mafuta, na eneo limetengwa rasmi kwa ajili ya shughuli hiyo sioni sababu ya kusitisha ujenzi wa kituo hicho. Kama ni sababu za kiusalama zilizowafanya kusitisha ujenzi wa kituo hicho cha mafuta sina shaka nalo lakini kama mmesitisha kutokana na ushauri kwamba maeneo ya jirani na stendi kuna kituo cha mafuta basi Miji mingine isingekuwa na vituo vya mafuta maana kila sehemu vipo mimi nadhani hiyo ya kuwepo kwa vituo vya jirani sio hoja.’’Jafo alifafanua

Jafo aliendelea kusema “Swala la msamaha wa VAT ni changamoto inayoikabili miradi mingi inayosimamiwa na TAMISEMI. Hapa Njombe naona tena changamoto hii inajirudia licha ya Mheshimiwa Rais kutoa maelekezo kuhusiana na suala hili. Naomba nichukue changamoto hii na nitaiwasilisha kwa Waziri wa Fedha kwa utekelezaji. Mimi nataka Halmashauri hizi zifuzu na kufikia uchumi wa kujitegemea.”Alisema

Naye Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Ruth Msafiri amemuahidi Mheshimiwa Jafo kuendelea kusimamia kwa ushirikiano shughuli zilizosalia za ujenzi na kumwambia kuwa pale patakapohitaji msaada hawatasita kuwasiliana kwa ajili ya kuhakikisha kuwa changamoto zinatatuliwa ili Wananchi wa Njombe waweze kunufaika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda amemshukuru Mheshimiwa Jafo kwa kutembelea mradi wa soko na kukagua shughuli za uendeshaji wa stendi na kuahidi kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Waziri huyo katika ziara yake.

“Sisi tutaendelea kusimamia kazi hizi kwa nguvu zote. Tutakuwa na vikao kila wiki kuangalia hatua ya namna gani tunamaliza shughuli za soko. Kuhusu wazo la kuendelea na ujenzi wa kituo cha mabasi ndani ya stendi tutaangalia sheria, kanuni, taratibu na hali za kiusalama kama vyote vinaruhusu tuone namna ya kurejesha ule mradi katika stendi yetu mpya.”Alisema Mwenda.

Mradi wa ujenzi wa stendi unatarajiwa kuingizia Halmashauri mapato ya zaidi ya milioni mia mbili hamsini kwa mwaka  huku mradi wa soko ukitarajiwa kuingiza zaidi ya milioni mia tatu kwa mwaka pindi itakapokamilika.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe