• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Jafo afurahishwa ujenzi wa Vituo vya Afya Njombe Mji

Tarehe iliyowekwa: December 22nd, 2020

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo amefurahishwa na ujenzi wa Vituo vya Afya Kifanya na Makowo ambapo asilimia kubwa ya ujenzi wa vituo hivyo unatekelezwa kutokana na makusanyo ya mapato ya ndani na nguvu za Wananchi ambapo zaidi ya Shilingi  milioni mia saba za mapato ya ndani zimepelekwa kwenye vituo hivyo.

Akizungumza Mara baada ya kukagua shughuli za Ujenzi Katika Kituo cha Afya Kifanya ambapo Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alikipatia kituo hicho kiasi cha Shilingi Milioni kumi kusaidia ujenzi, Waziri Jafo amesema kuwa jitihada zilizofanyika kupitia makusanyo ya mapato ya ndani kwa kujenga vituo vya afya viwili ni kubwa na amezitaka Halmashauri nyingine kuiga Mfano huo.

“Kituo ni kizuri na Kimejengwa kwa mapato ya ndani.Tunavyozungumza juu ya vituo vya afya 487 sasa tunakwenda mpaka vituo mia tano. Ninyi Mko vizuri. Niwapongeze kwa kazi kubwa mliyofanya Mimi nimeona kuwa mnafanya kazi nzuri endeleeni na kasi hii. Majengo haya yanakwenda kuwahudumia Wananchi .Hata ukienda kukusanya ushuru Mwananchi anakuelewa. Sio unakwenda kukusanya ushuru lakini matokeo yake hayaonekani.Naomba niwapongeze. Mnyonge Mnyongeni lakini Haki yake mpeni”Alisema Waziri Jafo.

Jafo anaendelea kusema licha ya kuwepo na kasi ya ujenzi Vituo vya Afya Serikali  pia imeendelea kutoa ajira kwa Wataalamu wa Sekta hiyo ili kuhakikisha kuwa vituo hivyo vinafanya kazi na kutoa huduma iliyo bora ambapo zaidi ya Wataalamu wa Afya elfu kumi na mbili (12,000)waliweza kuajiriwa katika kipindi hiki kwa awamu tofauti.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Deo Mwanyika na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda  wamemshukuru Waziri Jafo kwa kuweza kukagua ujenzi wa kituo hicho ambapo katika ziara hiyo ameweza kufanya mawasiliano na Katibu Mkuu TAMISEMI ili kuweza kupata vifaa  katika kituo hicho.

“Mheshimiwa Rais alituchangia milioni 10, Wananchi Wamechangia milioni 28 Halmashauri ya Mji Njombe imechangia milioni 370 ambapo sasa tupo katika hatua za mwisho za umaliziaji. Makadirio yetu ni milioni 420 kukamilisha ujenzi ambao utakuwa msaada mkubwa kwa Wakazi wa ene la Kifanya na maeneo ya jirani.”Alisema Mwenda.

Naye Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Deo Mwanyika anasema”Mheshimiwa Jafo ametutia moyo sana nilimweleza juu ya uwepo wa vituo vya Afya viwili Kifanya na Makowo.Tumemwomba Vifaa. wakati wa Kampeni niliwaambia Wananchi Serikali imejenga kituo cha Afya na tutahakikisha kuwa kinapata vifaa na Wataalamu wakutosha na tumepata majibu ya vifaa. Tunashukuru sana.Wananchi wa Kifanya watambue sasa Serikali yao ipo kazini.”

Awali katika ziara hiyo Mheshimiwa Jafo alipata nafasi ya kuzungumza na Watumishi kutoka katika Halmashauri ya Mji Njombe ambapo amesisitiza suala la ukusanyaji mapato na kufanya matumizi sahihi na amewataka wakurugenzi wote Nchini kuhakikisha kuwa ifikapo Mwishoni mwa mwezi Desemba Halmashauri zote 185 ziwe zimekusanya zaidi ya asilimia 50 ya lengo ambapo tarehe 15 Januari atatoa taarifa ya ukusanyaji mapato kwa kila Halmashauri  kwa kipindi cha miezi sita. Pia amewataka Wakurugenzi kuhakikisha kuwa fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi ya elimu madarasa na mabweni ifikapo tarehe 30 Desemba miradi iwe imekamilika.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe