Wito huo umetolewa na Afisa Ustawi Halmashauri ya Mji Njombe Petro Mahanza ambapo ameitaka jamii kuacha tabia ya kuwaficha Walemavu kwani Serikali imeweka miongozi ya kuwasaidia Walemavu kuanzia ngazi za Vijiji, Mitaa, Kata na Halmashauri.
Mahanza alisema kuwa ipo tabia ya baadhi ya Wanafamilia wanapokuwa na ndugu ambaye anaulemavu wamekuwa wakiwaficha na wakati mwingine kushindwa kutoa ushirikiano kwa Maafisa Ustawi ili kuweza kuwatambua jambo ambalo limekuwa likifanya makundi haya kushindwa kupatiwa misaada mbalimbali vikiwemo vifaa mbalimbali na badala yake wamekuwa wakifichwa ndani.
Akikabidhi misaada kwa walemavu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Kuruthum Sadick amesema kuwa kwa mwaka 2022/2023 Halmashauri imetenga Milioni 6 kwa ajili ya kuwasaidia Walamavu ambapo mpaka sasa kiasi cha Shilingi milioni tatu kimetumika kwa ajili ya kununua vifaa vilivyokabidhiwa na amesema kuwa matamanio yake ni kuona kila Mlemavu anaweza kufikiwa na kusaidiwa na pia kulingana na makusanyo ya mapato ya Halmashauri bajeti zaidi itaongezwa kwa kadri ya mahitaji kusaidia makundi hayo.
Aidha Kuruthum amewataka Wanafunzi wote ambao wenye ulemavu kuhakikisha kuwa Wanasoma kwa bidii kwani kuwa na ulemavu sio sababu ya kuwafanya kushindwa kufanya vizuri na amesema kuwa Halmashauri kupitia Kitengo cha Ustawi wa jamii kuhakikisha kuwa Watoto wenye ulemavu waliopo shuleni wanawezeshwa kwa kuwa na mazingira bora ya kusomea.
Chervin Mwalongo ni Mwanafunzi katika Shule ya Sekondari Makambako na ni mlemavu wa viungo ambaye yeye ameishukuru Halmashauri kwa msaada huo na amesema kuwa jamii isichoke kuendelea kusaidia makundi hayo kwani wapo wengi ambao hawajaweza kufikiwa.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe