Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mheshimiwa Erasto Mpete,ametoa rai kwa jamii kubadili tabia ili kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi na kuhakikisha maambukizi mapya ya ugonjwa huo yanatokomezwa kabisa mjini Njombe.
Mheshimiwa mpete ametoa rai hiyo kwenye ufunguzi wa mkutano wa robo ya kwanza wa baraza la madiwani uliofanyika Oktoba 31,2023 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe
Ameeleza kuwa hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa sasa sio nzuri hivyo amezitaka jamii kuendelea kupiga vita maambukizi mapya.
Aidha amezisisitiza asasi za kiraia zinazohusika na mapambano dhidi ya virusi vya ukimwi hukakikisha zinasimamia kikamilifu ili kuhakikisha Njombe Ukimwi unapungua.
Kwa mujibu wa takwimu zilizopo kwenye vituo vinavyotoa huduma za matunzo na matibabu(CTC)Halmashauri ya Mji Njombe takribani watu 16,633 kati yao wanawake 10,835 na wanaume 5,798 wanaishi na virusi vya Ukimwi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe