Timu ya wanafunzi na wakufunzi kutoka chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) Dar es salaam,inayofanya ziara Mkoani Njombe ,imetembelea kitalu cha uzalishaji wa miche ya parachichi cha NEMES Green Garden kinachomilikiwa na mkulima Steven Mlimbila kilichopo Halmashauri ya Mji Njombe ,Mtaa wa Maheve kata ya Ramadhani.
Akizungumza baada kupokea taarifa ya mkulima huyo ,kiongozi wa msafara ambaye pia ni mkufunzi kwenye chuo hicho Brigedia Jenerali Erick Mhoro amesema wamefika Njombe kuona utekelezaji wa sera za Serikali kwenye sekta mbalimbali ikiwemo kilimo.
"Tumefika hapa tuone uzalishaji wa parachichi kunzia shambani na tunashukuru tumeona uzalishaji wa miche na parachichi, kilimo hiki kwa Njombe wamepiga hatua, hongera na niseme Mlimbila ni kijana wakuigwa" Alisema Jenerali E. Mhoro.
Amepongeza mzalishaji wa miche NEMES kwa kazi anayoifanya ambayo inonekana wazi kuwa na mchango kwenye pato la taifa kwani parachichi kutoka Njombe imejizolea sifa kwenye soko la kimataifa.
"Kazi ni nzuri na nimependa siyo mchoyo anawafundisha na wengine. Ni jambo jema kama tulivyoeleza watu wanakuja kujifunza hapa wakawe wazalishaji kama yeye au wakubwa zaidi" Aliongeza Brigedia Jenerali E. Mhoro.
Katika hatua nyingine amemhakikishia mkulima huyo kuwa jicho la Serikali lipo kwenye kilimo hivyo changamoto ambazo amezianisha zinafanyiwa kazi ikiwemo changamoto ya umeme wa uhakika ambayo itakuwa historia nchini Tanzania baada yakukamilika kwa bwawa kubwa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere .
Kwa upande wake Kanali Maiyo mwanafunzi kutoka nchini Kenya, amesema anachokifanya NEMES ni cha kuigwa na vijana ambao wanapitia changamoto ya kukosa ajira kwenye nchi nyingi duniani
Ametoa wito kwa wananchi Mkoani Njombe haswa Vijana kuendelea kujihusisha na shughuli za kilimo hasa kilimo cha parachichi na miti kwa ajili ya mbao kwani wafanyabiashara wengi kutoka nchini Kenya hununua mbao na parachichi zinazozalishwa Njombe.
Steven Mlimbilia ( NEMES) ni miongoni mwa wakulima wakubwa wa Prachichi Mkoani Njombe alieamua kujikitika kwenye kilimo hicho tangu mwaka 2010 na mpaka sasa anamiliki hekari 180.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe