Mei 28,2024,Wananchi wa kijiji cha Luponde wameshuriwa kupima afya mara waonapo dalili za ugonjwa wa kifua kikuu.
Ushauri huo umetolewa na Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma Halmashauri ya Mji Njombe Dkt. Mashaka Kisulila wakati akitoa elimu ya kifua kikuu (TB), tohara na Ukoma kwa wakazi wa kijiji cha Luponde walioshiriki siku ya afya na lishe ya kijiji(SALIKI) iliyofanyika kijijini hapo.
Dkt. Kisulila amesema huduma ya upimaji na matibabu ya kifua kikuu hutolewa bure hivyo endapo mtu yeyote atapata dalili ikiwemo kikohozi cha wiki 2 au zaidi, kupungua uzito, watoto wadogo kutoongezeka uzito, kukosa hamu ya kula, Homa n kutokwa na Jasho jingi nyakati za usiku, afike kwenye kituo cha kutolea huduma za afya ili aweze kufanyiwa vipimo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe