Wajasiriamali wadogo,mkoani Njombe wameanza kuona matokeo chanya ya mikopo ya asilimia 10% ya Halmashauri, ambapo zaidi ya shilingi bilioni 21 zimeweza kutolewa kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi.
Akizungumza Agosti 26, 2025 Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Juma Sweda, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa Njombe Mhe. Anthony Matka katika kikao na wajasiriamali wadogo amesema vikundi 9109 kutoka mwaka 2021 hadi 2025 vimeweza kupatiwa mikopo ambayo imesaidia kuanzisha biashara ndogo, kununua vifaa vya kazi, na kuongeza mapato ya kaya.
Akiendelea kuzungumza na wafanyabiashara hao wadogo Mhe Sweda amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kuhakikisha mikopo inasimamiwa kwa uwazi na uadilifu, ili malengo ya kuboresha maisha ya wananchi yatekelezwe.
“Mikopo ni fursa kubwa kwa wajasiriamali, lakini lazima itumike kwa malengo yaliyokusudiwa. Maafisa wa maendeleo ya jamii watoe elimu sahihi na wahudumishe wananchi kwa heshima,” alisema Mhe. Sweda.
Serikali inaendelea kusisitiza kuwa mikopo hii, pamoja na mafunzo na uwezeshaji mwingine, ni chachu ya maendeleo ya kiuchumi, kupunguza umasikini, na kuongeza thamani ya bidhaa na huduma
katika halmashauri.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe