Wakizungumza mara baada ya kukagua na kutembelea mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Utalingolo kamati hiyo imebaini kuendelea kusuasua kwa ujenzi wa shule hiyo jambo ambalo linaweza kupelekea shule hiyo kutokamilisha ujenzi wa majengo muhimu kwa wakati kutokana na ukosefu wa mpango kazi wa shughuli za ujenzi katika shule hiyo.
“Shule hii imechukua muda mrefu sana katika ujenzi. Tumeona kunashughuli zinazoendelea za ujenzi. Kuna ujenzi wa majengo ya maabara, nyumba za waalimu, na Hosteli ya Wanafunzi shughuli hizi haziwezi kwenda kwa wakati mmoja na tunaona kuwa uchangiaji hapa wa Wananchi si wakuridhisha. Ni vyema wakaona yale ya msingi ili shule iweze kufunguliwa wakayapa kipaumbele kwanza. Wanafunzi wa Kata hii wanahangaika sana lakini pia Wananchi wa Kata hii si wa moja katika kuchangia inabidi waone ni kwa kiasi gani wanafunzi wanaofaulu katika Kata hii wanahangaika na itakapokamilika itakuwa mkombozi mkubwa” Alisema Mwanzinga Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha
Aidha katika Ujenzi wa Kituo cha Afya Kifanya na Ujenzi wa Madarasa katika Shule ya Msingi Mikongo Kamati pia imebaini kusimama kwa mradi kwa kipindi kirefu kutokana na Mwamko hafifu wa Wananchi kuchangia miradi hiyo na Waheshimiwa Madiwani wa Kata husika ambao ndio Wenyeviti wa Kamati za Maendeleo za Kata kutoshiriki ipasavyo kuhakikisha kuwa miradi hiyo inaendelea.
“Mheshimiwa Diwani unapaswa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia miradi inayotekelezwa kwenye Kata yako. Yapo maeneo ambayo miradi imesimama na fedha zipo lakini Madiwani hawafanyi jitihada za kusimamia miradi hiyo. Inabidi tutafakari nafasi tulizokalia na kuona kama tunawatendea Wananchi yale tuliyowaahidi. Alisema Mtamike Diwani wa Kata ya Mjimwema.
ziara hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Edwin Mwanzinga, Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Mkurugenzi wa Halmashauri na Wataalamu ilifanikiwa kutembelea miradi 12 katika sekta ya Afya na Elimu sambamba na kukagua shughuli za uendeshaji katika eneo la stendi mpya ya mabasi Njombe ambapo mradi wa ujenzi wa madarasa shule ya sekondari Matola, Ujenzi wa bweni Shule ya Sekondari Anne Makinda, Nyumba ya Mganga Iduchu na Ujenzi wa Zahanati Iduchu imeonekana kuwa katika hatua nzuri za ukamilishaji
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe