Wajumbe wa Kamati ya fedha Halmashauri ya Mji Njombe wamekagua shughuli za ujenzi wa miradi inayoendelea katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri na kuhimiza ubora na kasi katika ukamilishaji wa miradi hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya fedha Erasto Mpete akizungumza wakati wa ukaguzi huo amewataka Wasimamizi kwenye miradi kuhakikisha kuwa miradi hiyo inazingatia ubora uliokusudiwa na pia inakamilika kwa muda ili iweze kutoa huduma iliyokusudiwa kwa Wananchi.
Akizungumza katika ziara hiyo Angela Mwangeni Mjumbe wa Kamati ya fedha amepongeza Kazi kubwa inayofanywa na Serikali katika kuwaletea Wananchi wake Maendeleo na pia amesisitiza juu ya utunzaji wa kumbukumbu zote muhimu katika kila mradi husika ili kuweka wazi na kutoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya fedha katika mradi husika.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na Ujenzi waVituo vya AfyaLuponde na Mjimwema, Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa kupitia fedha za Serikali Kuu(Pochi ya Mama) na Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Lunyanywi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe