Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) imekagua na kutembelea katika Stendi ya Mabasi Njombe na Soko Kuu Njombe lengo ikiwa ni kujiridhisha na utekelezaji wa matumizi ya fedha zilizotengwa kwenye miradi hiyo.
Akizungumza wakati wa kupokea taarifa za utekelezaji wa miradi hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (LAAC) Grace Tendega amesema kuwa licha ya kuwa Kamati hiyo inalengo la kuangalia ni kwa namna gani fedha zilizotengwa kwenye miradi zinatumika lakini pia kamati inalengo la kuhakikisha kuwa kero zilizopo kwenye utekelezaji wa miradi hiyo zinapatiwa ufumbuzi kwa kufanya utatuzi na hivyo kufanya miradi iliyokusudiwa na Serikali kwa Wananchi kuwa endelevu na kuwa na tija kwa Wananchi.
Akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa mradi wa Stendi na Soko Afisa Mipango wa Halmashauri Shigela Ganja amesema kuwa Halmashauri ya Mji Njombe imefanikisha utekelezaji wa Ujenzi wa Stendi na Soko kupitia Programu ya Uimarishaji na Uboreshaji Miji (ULGSP) na hivyo kufanikiwa kupata kiasi cha Shilingi Bilioni 20 ikiwa ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo jambo ambalo liliepusha Halmashauri kuendelea na wazo na kukopo kwenye taasisi za kifedha ambazo pengine zingeweza kuwa na riba kubwa kwenye urejeshaji wa mkopo huo.
Aidha Ganja amesema kuwa licha ya kuwa Mradi wa Stendi na soko imebadili mandhari ya Mji na kuwezesha mazingira bora ya kutolea huduma, bado changamoto ya utekelezaji wa mradi wa stendi umeshindwa kuzaa matunda yaliyokusudiwa kutokana na kuwepo na stendi katikati ya Mji jambo linalopelekea abiri wengi kuishia mjini na stendi kushindwa kufanya kazi na kukusanya kwa kadri ya malengo Halmashauri iliyojiwekea.
Changamoto hiyo ya ufanisi wa stendi ukawaibuwa Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamatai hiyo kuoneshwa kutoridhishwa kwao na utendaji wa stendi hiyo ikiwemo idadi ya mabasi, Wananchi wanaotumia stendi hiyo na vibanda kushindwa kukodishwa .
Akizungumza katika kikao cha majumuisho mara baada ya kutembelea na kukagua miradi ya stendi na soko kuu ambayo miradi hiyo imeanza kutumika Mwenyekiti wa Kamati hiyo Grace ametoa maelekezo kwa Halmashauri kuhakikisha kuwa viongozi kwa kushirikiana na Halmashauri unakubaliana kutotumia stendi ya mabasi iliyopo mjini kwani inahatarisha usalama wa abiria na Wananchi na inaweza kusababisha maafa kwani stendi hiyo ipo kwenye hifadhi ya barabara na katikati ya Mji.
“Halmashauri mhakikishe kuwa katika katika maeneo yenye kasoro za ujenzi zikiwemo nyufa kwenye barabara za magari makubwa stendi kuu , na sakafu katika jengo la mama ntilie zinarekebishwa kufikia mwezi Juni. Aidha Mhamasishe Wafanyabiashara kupanga katika fremu za maduka zilizosalia na kufanya marekebisho katika soko la Dodoma ili wafanyabiashara wengine waweze kuhamishiwa huko na tuweze kupunguza msongamano katika soko jipya.”Alisema Mwenyekiti
Aliendelea kusema “Kumekuwa na majanga ya moto katika masoko mengi katika siku za hivi karibuni. Niwaombe muhakikishe kuwa soko linakuwa na Bima na pia kuboresha miundombinu kwa ajili ya Watu wenye ulemavu katika soko kuu hususani kwenye huduma ya migahawa.”Alisema Grace
Licha ya changamoto hizo na mapendekezo kamati hiyo pia imetoa pongezi kwa Watendaji kwa kuweza kufanya utekelezaji wa miradi na pia imeishauri Halmashauri na Wataalamu kuendelea kuwa Wabunifu wa vyanzo vya mapato na pia kuhakikisha kuwa mashine za kukusanyia mapato zinatumika katika maeneo ya makusanyo.
Katika hatua nyingine Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Ally Mwinyi akitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya stendi mpya ya Njombe, amesema kuwa Chama cha Mapinduzi hakipo tayari kuona Mwananchi akionewa na Halmashauri ikipoteza mapato kwani Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa stendi mpya ya kisasa na kuelekeza matumizi ya stendi yaendelee kama ilivyokuwa wakati stendi ikiwa inaanza kwa kufuta kituo cha msaada cha sasa kilichopo stendi ya zamani na badala yake kutumia stendi kuu na vituo vilivyokuwa vimeainishwa vya Nundu,Kibena,Ramadhani na stendi mpya.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe