Ni katika ziara ya Kamati ya siasa CCM Mkoa wa Njombe ikiongozwa na Mwenyekiti wake Jassel Mwalala ambapo ilitembe katika mradi wa ujenzi wa shule mpya ya magufuli na jengo la upasuaji katika hospitali ya kibena lengo ikiwa ni kuangali uteklezaji wa ilani ya CCM.
Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa shule ya msingi Mratibu elimu Kata ya Ramadhan Fortunatus Mbilo amesema kuwa ujenzi huo ulifuatiwa maombi ya wanafunzi wa shule ya msingi ramadhan kwa hayati dkt john pombe mqagufuli katika ziara yake mkoani njombe ambapo wanafunzi hao waliomba bwalo la chakula na kuongezewa vyumba vya madarasa kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi iliyokuwepo katika shule ya Msingi Ramadhan ambapo Hayati Dkt Magufuli aliwajengea bwalo na vyumba vya madarasa na ndipo wananchi walipohamasika na kuendeleza ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na baadaye halmashauri kupitia mapato ya ndani ilisaidia kuendeleza ujenzi wa madarasa 6 ofisi na vyoo.
“Wananchi wa Mtaa wa Ramadhan waliunga mkono kwa ujenzi wa madarasa matatu ofisi moja na matundu 9 ya vyoo vya wavulana kwa gharama ya Shilingi milioni 35,248,400 ambapo Halmashauri ya Mji Njombe ilitoa kiasi cha Shilingi milioni 116,600,000 ambapo iliwezesha ujenzi wa madarasa 6 matundu 4 ya vyoo vya Waalimu,madawati 250 na matundu 11 ya vyoo vya kike.”
Wakizungumza mara baada ya kupokea taarifa hiyo na kukagua ujenzi huo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe Jassel Mwalala ameipongeza Halmashauri kwa ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Magufuli na ameishauri Halmashauri kuhakikisha kuwa inaanza michakato ya ujenzi wa nyumba za Watumishi katika shule hiyo.
“Niwapongeze kwa kazi nzuri mliyoifanya kazi inavutia. Kwenye taarifa yenu nimeona kuna vyumba vimekamilika lakini havina madawati na kuna maeneo kuna madawati.Hivyo Mkurugenzi inabidi uandike kutoa maelekezo ya fedha kuelezea kuwa tumefanya mabadiliko kwenye mradi. Hatuwezi kuwa na madarasa yamekamilika na madawati yapo huko inabidi tufanye hivi ili watoto wetu waendelee kusoma.”Alisema Mwalala
Naye Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Rubirya ameelekeza katika kila mradi kuhakikisha kuwa kunakuwepo na taarifa ya mchanganuo wa fedha kwa kila chanzo na jinsi zilivyotumika ili kuweka uwazi zaidi kwenye utekelezaji wa miradi hiyo.
Aidha katika Hatua nyingine Kamati ya CCM Mkoa wa Njombe ilifika katika Hospitali ya Kibena ambapo imefanikiwa kufika katika jengo la upasuaji katika hospitali hiyo ambalo jengo hilo limeanza kutumika na kuipongeza Unicef kwa kufanikisha ujenzi wa jengo hilo kwa kushirikiana na Halmashauri nna Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo mpaka sasa jumla ya wakinamamam waliofanyiwa upasuji toka kuanza kutumika ni wanawake 12.
Katika hatua nyingine Mwalala ameupongeza uongozi wa Hospitali ya Mji Kibena kwa jinsi walivyojipanga kwenye utoaji wa huduma bora na jinsi walivyoweza kuboresha mazingira ya Hospitali hiyo ambao ni kongwe.
Kamati ya Siasa CCM Mkoa wa Njombe ipo katika ziara ya kukagua na kujionea utekelezaji wa Ilani ya CCM unavyofanyika katika Mkoa huo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe