Kamati ya Siasa Mkoa wa Njombe, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe (MB), Mhe. Deo Sanga, Octoba 11,2023 ilifanya kikao cha majumuisho ya ziara iliyofanywa na kamati hiyo kwa siku tisa (9) kwenye Halmashauri zote zinaunda Mkoa wa Njombe.
Ziara hiyo ililenga kutembelea na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Mji Njombe na Makambako na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe,Makete,Ludewa na Wangingombe.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe, Mhe. Deo Sanga, alisema kuwa katika ziara waliyoifanya ambayo ilipitia kata 81 nakukagua miradi 81 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 43.601 ilikuwa ziara nzuri iliyowaonesha kazi kubwa na nzuri sana ambayo inafanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya Afya ,Elimu,Miundombinu na Maji.
Pamoja na kazi nzuri iliyofanyika kwenye miradi iliyokaguliwa Mhe Sanga amesema, wamebaini changamoto kwenye baadhi ya maeneo nakutoa maelekezo kwa watendaji wa Serikali kupitia taasisi idara na vitengo kwenye halmashauri kuhakikisha zinafanyiwa kazi ili kuondoa malalamiko kwa wananchi.
"Tumegundua kuwepo kwa changamoto katika sekta ya Elimu na Afya hususani uwepo wa maboma ambayo ni viporo yanahitaji kukamilishwa na kuanza kutoa huduma , hivyo serikalini kupitia Halmashauri zote ziweke mkakati wa kukamilisha kwa haraka maboma hayo ili wananchi waweze kuhudumiwa kiufasaha" Alisema Mhe Sanga.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Antony Mtaka, amewataka watendaji wote kwenye Halmashauri kuwajibika na kuhakikisha wanatoa kipaumbele kwenye miradi viporo hasa ile iliyoanzishwa muda mrefu ili ikamilishwe na kuanza kutoa huduma inayotakiwa .
Naye Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Pindi Chana , amewataka watumishi wote wa Serikali kutimiza wajibu wao kikamilifu sambamba na kutii sheria ili kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) sambamba na kutii sheria.
Kikao kazi hicho kiliwahusisha Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya, Kamati ya Usalama ya Wilaya, Wakurugenzi watendaji pamoja na zao, pamoja na wasimamizi wa Taasisi mbalimbali Serikali kutoka kwenye kila Wilaya.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe