Agosti 21, 2025 - Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya Njombe ikiongozwa na Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Njombe, OCD Masoud Kwileka, imekagua miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi milioni 759,680,028 inayotekelezwa katika Halmashauri ya Mji wa Njombe.
Akizungumza mara baada ya kukagua miradi hiyo, OCD Kwileka ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Njombe, alisema ameridhishwa na namna mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe anavyosimamia utekelezaji wa miradi ambapo alisema juhudi hizo ni jambo linalotia moyo kwa wananchi wa maeneo husika.
Aidha ameipongeza timu ya wataalamu kutoka ofisi ya mkurugenzi na kuwataka waendelee kusimamia kwa karibu na kuhakikisha changamoto zinazoibuka wakati wa utekelezaji zinapatiwa ufumbuzi wa haraka.
“Niwapongeze sana mkurugenzi na timu yake kwa kusimamia vizuri miradi hii Endeleeni kusimamia kwa umakini ili iweze kukamilika kwa wakati na wananchi waanze kuitumia miradi hii ambayo ni kiu yao ya muda mrefu,” alisema OCD Kwileka.
Kamati hiyo ilikagua ujenzi wa madarasa 2 na matundu ya vyoo 12 shule shikizi ya msingi Nundu,ukamilishaji wa zahanati ya Itipula ,ujenzi bweni shule ya sekondari Kifanya na ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Magoda.
Miradi hiyo imetelezwa na fedha kutoka Serikali kuu,mapato ya ndani,B0OOST SEQUIP na mfuko wa jimbo ambapo mpaka sasa miradi bado inaemdelea kukamilika.
Ukaguzi huo umetajwa kuongeza uwajibikaji kwa wataalamu na viongozi wa halmashauri kwani dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kila mradi unaotekelezwa na kuleta tija kwa wananchi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe