Septemba 11,2024 ,Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Justine Nyamoga ilikagua nakuridhishwa na utelekezaji wa miradi ya Afya katika Halmashauri ya Mji Njombe.
Kamati hiyo ilikagua utekelezaji wa miradi miwili ya afya ambayo ni ujenzi wa kituo cha Muungano Kifanya na jengo la mama na mtoto lenye chumba maalumu kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati katika hospitali ya Mji Njombe Kibena iliyojengwa kwa fedha zaidi shilingi milioni 770 ikiwa ni fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri, TASAF,Michango ya wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo.
"Tumekagua na tumeridhishwa sana na huduma pamoja na uwepo wa vifaa vilivyo katika miradi hiyo. Vifaa na miundombinu vimetekelezwa kwa kiwango kinachokubalika na vinatimiza mahitaji ya jamii husika."Alisema Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe.Justine Nyamoga.
Aidha, kamati hiyo imewapongeza watumishi wa Halmashauri ya Mji Njombe wakiongozwa na Mkurugenzi wake Bi.Kuruthum Sadick kwa kujitoa na kujitolea kuhakikisha kuwa miradi inatekelezwa kikamilifu katika bora unaotakiwa.
Kamati hiyo imetoa wito kwa watendaji wote kuendelea kujituma ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na huduma bora, hususani katika sekta ya afya, ikiwemo kuweka mazingira ya uzazi salama.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe