Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Compain) Mkoa wa Njombe utaambatana na zoezi la utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwenye kata na vijiji katika Halmashauri zote sita za Mkoa wa Njombe.
Hayo yamebainishwa Mei 24,2024 na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu, baada ya kutambulishwa na mkuu wa wilya ya Njombe Mhe.Kissa Kasongwa kwa wananchi na watendaji wa kata 13 za Halmashauri ya Mji Njombe waliofika ofisini kwake kupata huduma mbalimbali ikiwemo msaada wa kisheria
“Tuko hapa Njombe kwa ajili ya tukio kubwa la uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia(Mama Samia Legal Aid Compain) mkoa wa Njombe, katika kampeni hii tutakwenda kwenye Halmashauri zote na huko tutatoa huduma katika kata 10 na vijiji visivyopungua 3”.Alisema Dkt.Kazungu.
Dkt.Kazungu ametoa wito kwa wananchi wote wenye changamoto mbalimbali zinazohitaji msaada wakisheria kujitokeza ili zitatuliwe.
“Tumefika na timu ya wataalamu wakutosha kutoka Wizara ya Katiba na Sheria,Maendeleo ya Jamii na dawati la jinsi na timu hii itatoa msaada wa kisheria kwenye masuala ya mirathi, ndoa, migogoro ya ardhi pamoja na matatizo ya unyanyasaji wa kijinsia, kwa matatizo ambayo yatashindwa kutatuliwa wahusika watapatiwa wakili bure kwa ajili yakuendelea na taratibu nyingine za kisheria.”Alieleza Dkt.Kazungu.
Kata za Halmashauri ya Mji Njombe zitakazofikiwa na huduma ya msaada wa kisheria ni kata ya Mjimwema,Njombe Mjini,Ramadhani,Lugenge ,Yakobi,Kifanya,Iwungilo,Ihanga,Luponde na kata ya Uwemba.
Pamoja na huduma ya msaada wa kisheria zitatolewa huduma za upimaji wa afya bure kwa Saratani ya mlango wa kizazi, Saratani ya matiti, tezi dume, uchunguzi wa sikio, pua na koo pamoja na upamaji wa magonjwa mengine yasiyoambukizwa. Huduma zote zitatolewa na madaktari bingwa kutoka hospitali ya Aghakhan.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe