Wananchi wa kata ya Njombe mjini wametakiwa kulima mbogamboga katika maeneo ya makazi yao na kuzingatia Lishe bora yenye mchanganyiko wa makundi yote matano ya chakula.
Wito huo umetolewa Novemba 24,2023 katika mitaa mitatu ya Njombe Mjini ambayo ni Mtaa wa Posta, Mtaa wa Sido na Buguruni ambapo Bwana .Enos Lupimo Mtendaji wa Kata ya Njombe Mjini amesema hali ya udumavu Mkoani Njombe ni mbaya ambapo asilimia 50% ya watoto wamedumaa kutokana na kutopata lishe bora.
Bwana Lupimo ameomba wazazi na walezi wote kuhakikisha lishe bora ili kuweza kutokomeza udumavu kwa Mkoani Njombe
Sambamba na hilo Bw. Lupimo ameshauri kupanda miche kuanzia miti miwili ya parachichi na kupanda mbogamboga katika maeneo ya makazi yao.
Naye Tumani Mtewa Diwani wa viti maalumu kata ya Njombe Mjini amewaomba wanawake mkoani Njombe kutotumia muda mwingi katika kazi zao badala yake wajikite katika malezi ya Watoto kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa lishe.
Kwa upande wake Polisi wa kata kaya Njombe mjini Florida Kiecha amewataka wazazi kujenga urafiki na watoto ili kupata taarifa endapo mtoto atafanyiwa ukatili wa kijinsia pamoja na kuwapa malezi bora.
Kauli mbiu ya kutokomeza udumavu katika kata ya Njombe mjini inasema“afya yangu ,lishe yangu lishe yangu afya yangu”
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe