Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amemtaka msimamizi wa ghala la kuifadhia mbolea zinazozalishwa na kampuni ya Itracom Fertelizer Tanzania yenye makao makuu yake Mkoani Dodoma,kuhakikisha anakuwa mzalendo na kuwa mwaminifu katika kazi yake.
Mheshimiwa Mtaka amezunguma hayo Novemba 10,2023 baada yakufanya uzinduzi wa ghala lakuhifandhia mbolea za kampuni hiyo ya Intracom lililojengwa mtaa wa kambarage kata ya Njombe Mjini.
Mtaka amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wasimamizi wa maghala kukosa uaminifu kwa sababu ya tamaa jambo ambalo limewaumiza baadhi ya wakulima mkoani Njombe.
“kampuni imekuamini kwa uaminifu mkubwa, ninyi wenyewe watanzania mnakatisha watu tamaa ,unakuja unamfanyia binadamu mwenzako matendo ya kinyama,hatutarajii ufike kwenye tamaa yakijinga ya namna hiyo, fedha zinapita unakufa unaziacha”Alisema Mhe Mtaka.
Aidha ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kupitia kitengo cha masoko kuweka mkakati wa masoko haswa kwa mkoa wa Njombe ambao ni mkoa wa pili kwa matumizi ya mbolea nchini Tanzania ,ili kuongeza mauzo na kuwezesha kampuni hiyo kuendelea kuzalisha mbolea kwa wingi nakutimiza maono ya Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha nchi inakuwa na viwanda vya kuzalisha mbolea nakuacha kuagiza mbolea kutoka nje ya nchi kwa gharama kubwa.
Amesema ipo haja kwa wakulima mkoani Njombe kuwa na uelewa mkubwa wa mbolea hiyo inayozalishwa hapa nchini kwa kutumia malighafi za ndani ikiwemo samadi ambayo hufanya ardhi kukaa na rutuba kwa muda mrefu na hivyo kupunguza matumizi ya mbolea mbadala kwa kiwango kukubwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe.Erasto Mpete ametoa rai kwa kampuni hiyo kuhakikisha inakuwa na mashamba darasa kwenye kata zote ili kuonesha ufanisi wa mbolea hiyo kwa wakulima.
Kampuni ya Itracom fertilizer Tanzania ilianza rasmi kuzalisha na kusambaza mbolea Disemba 2022 na inazalisha mbolea aina 3 ambazo ni mbolea ya kupandia ,kukuzia na mbolea ya kunepesha kwa kuzingatia afya ya udongo.Mpaka sasa kiwanda kimefanikiwa kusambaza mbolea kwenye mikoa zaidi ya 18.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe