Katibu tawala Wilaya ya Njombe Ndugu Agatha Mhaiki amefanya ziara kwenye vituo vya kuuza mafuta (petrol station) mjini Njombe kujionea hali halisi ya utoaji huduma wakati ambao vituo vingi vinaripotiwa kushindwa kutoa huduma kutokana na uhaba wa mafuta.
Septemba 04 ,2023,Akiwa kwenye mojawapo wa vituo vya kuuzia mafuta mjini njombe katibu tawalaAgatha Mhaiki amekukagua visima vya kuhifadhia mafuta kituoni hapo kwa lengo la kuondoa sintofahamu kwa wananchi kuwa wamiliki wa vituo hivyo wameacha kutoa huduma kwa lengo la kusubiri bei ya mafuta kupanda .
Aidha ametoa rai kwa vyombo vya usafiri vinavyotoa huduma kwa wananchi kuendelea kufuata miongozo ya bei elekezi za nauli kwa kila kituo na kuwaomba kutotumia changamoto iliyopo kupandisha nauli kiholela.
Katika hatua nyingine amesema taarifa ya uhaba wa mafuta mkoani njombe tayari imewasilishwa kwa mamlaka husika na anaamini inafanyiwa kazi kwa umuhimu wake ili shughuli ziweze kurejea kama kawaida.
Katika ziara hiyo katibu tawala wilaya ya Njombe aliongozana na timu ya ulinzi na usalama wilaya ya Njombe pamoja na Afisa Biashara wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi .Upendo Mwankemwa na mpaka kukamilika kwake kati ya vituo zaidi ya kumi vilivyopo Njombe Mjini ni kampuni moja ya Oraxy ndiyo ilikuwa ikitoa huduma kwa watumiaji wa mafuta aina ya diesel.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe