Mnamo tarehe 21 Oktoba 2022,Halmashauri ya Mji Njombe kwa kushirikiana na Wakufunzi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI iliandaa mafunzo kwa Wenyeviti wote wa Mitaa na Vijiji ndani ya Halmashauri kwa lengo la kuwakumbusha majukumu yao pamoja kuongeza ufanisi katika utendaji wa majukumu yao ya kila siku.
Akizungumza wakati wa Mafunzo hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Kuruthum Sadick amewataka Wenyeviti kuhakikisha kuwa wanayatumia mafunzo hayo kurekebisha pale ambapo walikuwa wanakosea pamoja na kuongeza ufanisi zaidi kwenye utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Kuruthum alisema kuwa Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji ni kiungo muhimu katika maendeleo ya Halmashauri kwani wao ndio wenye watu na hivyo ni vyema kutumika vyema katika kuhakikisha jamii inakua na uelewa wa miradi inayotekelezwa katika Vijiji na Mitaa yao pamoja na kuwa washauri wema wa masuala mbalimbali wanayopelekewa mezani kwao badala ya kuwa wachochezi na wasababishi.
Akifungua mafunzo hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Erasto Mpete amewasihi Wenyeviti kuzingatia yale watakayokuwa wamefundishwa na kuyatumia mafundisho hayo kuleta mabadiliko chanya ndani ya Halmashauri na katika utendaji kazi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa National Housing Malaki Mwandila amesema kuwa wanaishukuru Halmashauri kwa kuwaandalia mafunzo hayo ambayo yatawakumbusha wajibu wao na pia kuwaongezea ufanisi katika kuwahudumia Wananchi
Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Mji Njombe kupitia Idara ya Utumishi na Utawala imekua ikiandaa mafunzo kwa makundi mbalimbali ambapo awali yalifanyika mafunzo ya Madiwani kwa lengo la kuongeza ufanisi na kukumbusha wajibu na majukumu yao katika utekelezaji wa kazi zao.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe