Mradi wa Ujenzi wa bweni la wavulana katika shule ya sekondari uwemba unaofadhiliwa na mfuko wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) kwa gharama ya shilingi Milioni 130,000,000/= Umeanza kwa wananchi pamoja na wataalamu kujitolea nguvu kazi katika hatua ya awali ya ujezi wa msingi.
Agosti 31 ,2023 ,Wanachi wa kijiji cha Ikisa Kata ya Uwemba wamejitokeza kwa wingi kushirikiana na viongozi wa kata pamoja na maafisa maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Mji Njombe, katika ujenzi wa msingi kwa jili ya Bweni la wavulana kwenye Shule ya Sekondari ya Kata ya Uwemba.
Christina Njogela ni Afisa Mtendaji wa kata ya Uwemba , amesema ujenzi wa bweni hilo utaboresha mazingira ya kuishi na kujifunzia kwa wanafunzi wa shule hiyo.Ametumia fursa hiyo pia kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu kwenye shule za sekondari nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Ikisa Leonard Mathias Kadaga amesema kwa sasa mwamko wa wananchi kujitoa kushiriki shughuli za maendeleo ni mkubwa na unachochewa zaidi na juhudi za serikali za kuhakikisha changamoto mbalimbali ndani ya jamii zinatatuliwa.
Naye afisa maendeleo wa kata ya Uwemba Frola Kapinga amesema kuwa Idara ya Maendeleo itaendelea kushirikiana pamoja na wananchi katika shughuli mbalimbali za maendelo ili kuamsha ari na kutoa hamasa kwa wananchi kuwa na utamaduni wa kushiriki shughuli za maendeleo kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.
Bweni linalojengwa litakuwa na uwezo wa kulaza wanafunzi themanini (80). Awali wanafunzi wavulana katika shule ya sekondari Uwemba walilazimika kutumia vyumba vya madarasa kama mabweni .
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe