Wadau mbalimbali wameombwa kujitokeza kusaidia ujenzi wa nyumba ya kuishi familia ya kijana muhitaji ambaye ni mlemavu Ismail Rashid Kinumbi ili kuwatoa kwenye adha wanayoipata kwenye nyumba za kupanga.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Njombe Mhe. Kissa Gwakisa Agosti 17,2023 wakati alipomtembelea kijana huyo nyumbani anapoishi kumjulia hali na kumkabidhi baadhi ya mahitaji yaliyotolewa na wadau pamoja nakuona hatua zilizofikiwa kwenye ujenzi wa nyumba kwa ajili ya hiyo.
Mhe Kissa ametumia fursa hiyo kuwashukuru wadau mbalimbali waliojitoa kwa nyakati tofauti akiwepo Mkurungenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Ndugu Kuruthum Sadick kwa kuhakikisha kijana Ismail anapata bima ya afya, kiti mwendo (wheelchair) pamoja na mahitaji mengine muhimu kulingana na hali yake ikiwemo diapers za kumsitiri na chakula.
Aidha ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi na wadau wengine walioweka ahadi za kumsaidia kijana huyo kuhakikisha wanazitimiza ili ujenzi wa nyumba yakuishi familia hiyo uendelee na kukamilika kwa haraka.
Mhandisi wa ujenzi Halmashauri ya Mji Njombe Bernadetha Mihambo amesema ujenzi wa nyumba hiyo unatarajia kutumia kiasi cha shilingi milioni 29,000,000/= akiomba wananchi kujitoa kwa moyo ili ujenzi wa nyumba hiyo uweze kukamilika.
Kwa upande wake mama mzazi wa kijana Ismail Bi Shakira Ngonyani ametoa shukrani zake za dhati kwa wale wote waliojitokeza kuchangia mpaka kukamilisha hatua ya ujenzi wa msingi wa nyumba ,kisima pamoja na uzio.
Kwa yeyote anayeguswa kuchangia ujenzi wa nyumba yakuishi kijana Ismail Kinumbi,michago yote inapokelewa na Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Mji Njombe Petro Mahanza kwa nambari ya Simu 0767 - 300801.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe