Mkurugenzi wa Halmashauri wa Mji wa Njombe Bi.Kuruthum Sadick Agosti 14,2024 amefanya kikao kazi na watumishi wote wa makao makuu ya Halmashauri ya Mji Njombe kwa ajili ya kuwapongeza kwa kumaliza mwaka wa fedha 2023/2024, nakumbushana mambo yakuzingatia kwenye utendaji katika mwaka wa fedha unaondelea wa 2024/2025.
Katika kikao hicho Bi.Kuruthum amesisitiza watumishi wote kufanya kazi kwa weledi, uadilifu uwajibikaji , ushirikiano na kuwa na mahusiano mazuri kazini ili kila mmoja kwenye nafasi yake aweze kufanikisha lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Aidha amepongeza utendaji kazi wa kila Idara na Vitengo kwa mwaka wa fedha uliopita wa 2023/2024 haswa katika ukusanyaji wa mapato ambao umewezesha Halmashauri kufanya ufuatiliaji na utelekezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo kwa wananchi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe