Oktoba 05,2025,Watumishi wa Kitengo cha Ardhi Halmashauri ya Mji Njombe wamefanya hafla fupi ya kumuaga na kumtakia kheri mtumishi mwenzao aliyekuwa akijitolea kama Afisa Ardhi Msaidizi tangu mwaka 2022.
Hafla hiyo imeongozwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo, Bw. Emmanuel Luhamba, ambaye ametumia nafasi hiyo kumpongeza mtumishi huyo kwa moyo wa kujitolea aliouonesha katika kipindi chote cha utumishi wake. Aidha, ametoa wito kwa mtumishi huyo kuendelea kuwa na bidii, uadilifu na uwajibikaji awapo kazini.
“Ni muhimu kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma ili kuendelea kujenga taaluma yenye heshima na kuaminika,” alisema Bw. Luhamba.
Kwa upande wake, mtumishi aliyeagwa Bw.David Jumbe ameishukuru Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe kwa kumpatia nafasi ya kujifunza na kupata uzoefu katika mazingira ya kazi Serikalini.Amewashukuru pia watumishi wenzake kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote cha utumishi wake wa kujitolea.
Hafla hiyo imeonesha mshikamano na ushirikiano miongoni mwa watumishi wa kitengo cha Ardhi huku wakisisitiza umuhimu wa kuthamini na kutambua mchango wa kila mmoja katika taasisi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe