Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, amesema matukio ya ajabu na yakutisha yanayotokea katika maeneo tofauti ya mkoa wa Njombe yanapaswa kukemewa vikali na kila mtu ili kulinda utu na kujenga taswira nzuri ya Mkoa wa Njombe.
Akizungumza Tarehe 19 Disemba 2024 ,wakati wa ufunguzi wa kikao kazi alichokiandaa maalum kwa ajili ya kujadili hali ya usalama katika Mkoa wa Njombe, Mhe Mtaka amesema lengo ni kujadiliana na kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana na matukio yanayofanywa na watu ambayo yanahatarisha usalama wa watu na kuharibu taswira ya Mkoa wa Njombe.
Mhe. Mtaka alisisitiza umuhimu wa wadau na jamii kwa ujumla kushirikiana katika kutafuta suluhisho la changamoto za kiusalama zinazokabili mkoa Njombe.
Ameeleza kuwa kila mtu katika nafasi yake ana wajibu wa kuchangia juhudi za kuimarisha usalama na kulinda heshima na utu wa binadamu katika jamii.
Kikao hicho kimewashirikisha wadau mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Kissa Gwakisa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, maafisa tarafa, viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa dini, watendaji wa kata na mitaa, maafisa ustawi wa jamii, wazee maarufu, viongozi wa kimila, pamoja na wawakilishi wa bajaji na bodaboda.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe