Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mheshimiwa Kissa Gwakisa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Njombe Bi. Agatha Mhaika wameungana na vijana 200 ambao ni wanufaika wa mpango wa fursa kwa vijana uliopo chini ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Njombe kujifunza kwenye shamba la kijana Erasto Mkiwa aliyewezeshwa na mradi wa Feed The Future kufanya kilimo cha Nyanya kwa kutumia kitalu nyumba (Greenhouse) katika kijiji cha Magoda kata ya Uwemba Halmashauri ya Mji Njombe.
Akiwa shambani hapo, Mhe. Gwakisa amewataka vijana kuchangamkia fursa zitakazotolewa na na Ofisi yake na kuwaonya watakao patiwa mikopo kuepuka tamaa na kuwa na nidhamu kwenye matumizi ya fedha.
“Vijana changamkieni hizi fursa zinazotolewa na serikali kwa kutumia fedha mnazopata kwa lengo lililokusudiwa,” alisema.
Kwa upande wake Afisa Kilimo kutoka shirika la misaada la Marekani USAID The Future Feed Kilimo Tija Bwana Simon Mabula alisema shirika lake litasaidia vikundi 10 vya vijana ambao watahitaji kujifunza shughuli za kilimo.
“Tutasaidia vikundi 10 vya kilimo kwenye kitalu nyumba (Green House) nakutoa mikopo ambayo itawasaidia katika kuwaingizia kipato katika wilaya ya Njombe,” alisema.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe