Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mkoa wa Njombe, Erasto Mpete ametembelea barabara Njengelendete hadi Utalingolo kilomita 10 inayotekelezwa kwa kiwango cha changalawe na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wilaya ya Njombe.
Pia ametembelea barabara ya Kilenzi, kisilo hadi Luponde kilomita 9 ambapo amempongeza Mhandisi wa TARURA Wilaya Njombe kwa kuhakikisha barabara zinatengenezwa vizuri kwa kiwango ambacho serikali inahitaji kwa wananchi.
Aidha Mpete ameuomba meneja wa TARURA kwamba katika ukarabati unaoendelea kuhakikisha wanamwaga maji mengi ili kuepukana na vumbi ambalo linaleta kero.
“Wote tunapenda maendeleo ya kuboreshewa kwa barabara zetu nikuombe Meneja wa TARURA waambieni wakandarasi ambao wanatekeleza ujenzi wa barabara, wanaposhindilia wamwage maji mengi ili kuepusha vumbi kwa wananchi,"amesema Mh Mpete.
Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini TARURA Wilaya Njombe, Costantine Ibengwe amesema halmashauri ya mji Njombe imetengewa shilingi bilioni 3.2 na serikali kwa ajili ya utekelezaji miradi ya barabara ambazo tayari zimeanza kufanya kazi za ukarabati wa barabara na baadhi ya maeneo korofi ambayo yameharibiwa na mvua.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe