Na Ichikael Malisa - Njombe
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Oktoba 26,2023 ametoa maelekezo kwa wizara ya afya pamoja na Bohari ya Dawa Tanzania MSD kuhakikisha inasimamia kiwanda chakuzalisha mipira ya mkono (gloves) mjini Makambako, ili kianze kufanya kazi ifikapo Januari Mosi 2024.
Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye kiwanda hicho Dkt. Mpango amesema serikali iliamua Kuja na Mpango wa kujenga viwanda kwenye sekta ya afya ili kupunguza uagizwaji wa dawa kutoka nje ya nchi.
Amesisitiza kuwa serikali ilikabidhi jukumu la kuzalisha, kununua, kutunza na kusambaza kwa bohari ya dawa Tanzania MSD ili kuongeza upatikanaji wa vifaa tiba kupungiza matumizi ya fedha kigeni pamoja na kuongeza soko la ajira kwa wa Tanzania.
Aidha ameigiza kuongezwa kwa idadi ya wafanyakazi kwenye kiwanda hicho hasa wanawake wanaotokea kijiji cha Idofi ili waweze kunufaika na mradi huo.
Katika hatua nyingine Dkt Mpango amewataka watumishi wa Bohari ya dawa kuwa wazalendo nakuzingatika maadili ya utumishi.
Kufutia ombi la kuwekwa lami barabara inayoelekea kiwandani hapo lililowasiliswa na Mbunge wa Makambako Mheshimiwa Deo Sanga, Mheshimiwa Dkt Mpango amesema;
"Tamisemi iagizeni Wakala ya barabara za mijini na vijijini TARURA wakamilishe tathmini ndani ya wiki mbili wawasilishe kwakuwa serikali yetu inayoongozwa na mama Dkt Samia Suluh. Hassan ni sikivu na ipo kazini hii kilometa 1 itajengwa kwa kiwango cha lami.
Pamoja na hilo ameita MSD kuzingatia misingi ya kibiashara ili iweze kujitegemea kwenye uzalishaji sambamba na kuhakikisha kiwanda cha Idofi kinazalisha bidhaa nyingine kama dawa na vitendnishi.
Aidha ameigiza kundaliwa kwa taarifa ya kina ya mitambo iliyopo kiwandani hapo ambayo haifanyi kazi kwa miaka miwili sasa samba samba na mkakati wa kujibu na kumaliza hoja za ukaguzi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe