Wananchi wote wa Mkoa wa Njombe na maeneo jirani, mnakaribishwa kwenye BONANZA KUBWA LA MICHEZO litakalofanyika tarehe 25 Oktoba 2025, kuanzia saa tatu asubuhi katika uwanja wa Sabasaba, Njombe Mjini.
Bonanza hili limeandaliwa na Halmashauri ya Mji wa Njombe likishirikisha timu na taasisi mbalimbali kutoka mkoa wa Njombe na Iringa zikiwemo ; Halmashauri ya wilaya ya Njombe ,Iringa Manispaa, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi,Halmashauri ya Mji Makambako, Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa,Kituo cha redio Kings FM, Njombe Veterans, na Twende Pamoja Veterans
Njoo ushuhudie burudani na ushindani wa hali ya juu kwenye michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, netball, volleyball, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, mbio za magunia.Meza ya bahati na sibu itakuwepo.
Mgeni rasmi kwenye Bonanza hilo atakuwa Mheshimiwa Antony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
Usipange kukosa, ni siku ya michezo, furaha na umoja wa kijamii.
Njoo tujumuike, tufurahie, na tuimarishe afya kupitia michezo.
"Kumbuka! Kura yako, haki yako Jitokeze kupiga kura".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe