Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Mhe .Chifu Deo Mwanyika amewataka wakazi wa mtaa Mpechi na Joshoni kuhakikisha wanatumia fursa zitakazo jitokeza wakati wa ujenzi wa Chuo Kikuu ambacho kitajengwa katika maeneo . .
Ameyasema hayo Januari 8 ,2024 akiwa katika mkutano wa kutatua kero za wananchi wa mitaa hiyo ambapo alitumia jukwaa hilo kuwa omba wananchi wa mitaa hiyo kuhakikisha wanatumia fursa za kibishara ili kuweza kujipatia kipato .
"Ndugu zangu wananchi wa Mpechi na Joshoni Chuo Kikuu kinajengwa katika eneo letunambalo lupo karibu na Shule ya sekondari Ya Njombe Sekondari (Njoss) sasa itakuwa ajabu ayoke mtu mkoa mwingine aje ajenge atumie fursa naninyi mkiwa hapahapa mtakuwa hamjakitendea haki chuo hiki "Amesema Mhe Deo Mwanyika Mbunge Jimbo la Njombe Mjini.
Akiendelea kuzungunza na wananchi hao Mbunge Mwanyika ameahidi kiasi cha shilingi Milioni moja kwa ajili ya kuleta umeme katika ofisi ya Mtaa wa Joshoni kutokana na ofisi hiyo kushindwa kufanya kazi za wananchi kwa wakati.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe amewataka wananchi wote wa mitaa hiyo kuhakikisha wanasafisha mazingira yao kwa wakati huku wanaouza malimbichi mitaani kuhakikisha wanahama maramoja ifikapo Februari 01,2024.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe