Na,Ichikael Malisa.
Jamii Mjini Njombe imehimizwa kuzingatia lishe bora na kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya zinaa haswa kwa wajawazito ili kukabiliana na changamoto ya watoto kuzaliwa kabla ya wakati(Njiti) na wenye uzito pungufu.
Wito huo umetolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Dr. Jabil Juma,ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya watoto Njiti duniani yaliyofanyika Tarehe 17 Novemba 2024 katika hospitali ya Mji Njombe Kibena.
Akizungumza na wazazi walioshiriki maadhimisho hayo Dr.Jabil alisisitiza umuhimu wa lishe bora kwa mama mjamzito na maandalizi sahihi kabla ya ujauzito.
"Tuambizane ukweli , lishe duni kwa wajawazito ni moja ya sababu kuu zinazochangia kuzaliwa watoto njiti ,maandalizi ya kuzaa yanapaswa kuanza mapema, ndani ya umri wa kuzaa. Mama mjamzito anapaswa kuwa tayari na kuhakikisha anapata lishe bora kabla ya kushika ujauzito," alieleza.
Alionya pia juu ya athari za maambukizi ya magonjwa ya zinaa, kama vile kaswende na VVU, akieleza kuwa yanahatarisha afya ya mama na mtoto jambo ambalo linaweza kusababisha mtoto kuzaliwa kabla ya wakati na mwenye uzito pungufu.
"Tukiamua kupambana na maambukizi haya kwa kujilinda na kuwa tayari kupima afya zetu mara kwa mara, itasaidia uzazi slama, tunapata ujauzito tukiwa na afya bora na kuzaa watoto wenye afya njema," aliongeza.
Aidha aliwataka wananchi kuendelea kutoa maoni ya namna huduma za afya zinavyotolewa katika hospitali ili kusaidia maboresho na huduma bora kwa jamii.
“Maoni yenu ni muhimu sana katika kuhakikisha tunaendelea kutoa huduma bora kwa jamii. Tutaendelea kuboresha mazingira yetu ili huduma hizi ziendelee kuwa bora.”
Maadhimisho ya siku ya watoto Njiti duniani 2024 yameongozwa na kaulimbiu inayosema, Kitendo kidogo,matokeo makubwa ikionesha umuhimu wa wazazi kutumia njia ya Kangaroo kusaidia ukuaji wa watoto Njiti.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe