Wajumbe wa Baraza la Madiwani wamepongeza wataalamu wa Halmashauri ya Mji Njombe kwa maandalizi mazuri ya taarifa ya Hesabu za Mwisho wa Mwaka wa fedha 2023/2024.
Wakizungumza kwenye kikao maalum cha kujadili na kupitisha taarifa hizo, madiwani hao akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe.Nestory Mahenge ,Diwani wa kata Njombe Mjini Mhe.Alatanga Nyagawa Diwani wa kata ya Yakobi Mhe.Michael Uhahula na Diwani wa Kata ya Ramadhani Mhe. Nickson Nganyange,walionyesha kuridhishwa na umakini na ufanisi wa wataalamu hao katika kuhakikisha taarifa hizo zinasomwa na kueleweka kwa urahisi.
Pia walisisitiza umuhimu wa kuendelea na juhudi hizo ili kuhakikisha uwazi na uwajibikaji katika masuala ya fedha za umma.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe