Machi 28,2024, Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba iliyopo Mkoa wa Morogoro wakiwa wameongozana na timu ya wataalamu wa Halmashauri hiyo,walifanya ziara ya kujifunza kwenye sekta ya kilimo katika Halmashauri ya Mji Njombe.
Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kujifunza kuhusu Kilimo cha zao la parachichi ambapo timu hiyo ilipatiwa elimu kuhusu Kilimo cha parachichi ikiwemo aina za parachichi zinazolimwa Njombe, namna ya kuandaa miche bora ya parachichi, namna bora ya kuandaa shamba, wakati na namna ya kupanda, kuhudumia shamba na miti kulingana na umri, mbinu za kukabiliana na magonjwa, uvunaji, masoko pamoja na changamoto mbalimbali kwenye Kilimo cha zao la parachichi.
Kiongozi wa msafara huo Emael Richard Ndangalasi, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, baada yakukamilika kwa ziara hiyo alitoa shukrani kwa ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe kwa kuwapokea na kufanikisha lengo la kujifunza Kilimo cha zao la parachichi.
Alieleza kuwa elimu ya kina waliyoipata kwa kushirikiana na wataalamu wataifikisha kwa wananchi haswa vijana ili waweze kuchangamkia fursa ya kilimo cha parachichi kwa kuwa jiografia na hali ya hewa ya Mlimba inaruhusu kulima parachichi badala ya kuangalia kilimo cha mpunga pekee kama zao la biashara.
Timu hiyo ilipata fursa ya kumtembelea shamabani mkulima na mzalisha wa miche bora ya parachichi Ndg. Steven Mlimbila anayemiliki zaidi ya hekari 200 za parachichi na kitalu chakuzlishia miche zaidi ya laki moja na nusu ambapo waliweza kupata uzoefu wa zaidi ya miaka kumi kutoka kwa mkulima huyo anayetambulika kwa jina la NEMES green garden.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe