Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Njombe leo imefanya Mkutano wa baraza kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa za utendaji kazi wa kila Kata kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2022/20223,ambapo kila Diwani aliweza kuwasilisha taarifa ya utekelzaji wa Kata yake hoja kuu ikiwa ni pongezi kwa Serikali kwa jinsi inavyotoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa miradi ambayo inaendelea katika kata 10 za Halmashauri ya Mji Njombe
Akifungua mkutano wa Baraza Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Filoteus Mligo amesema kuwa katika kipindi cha robo ya kwanza Halmashauri imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.3 na kusisitiza mkazo zaidi juu ya usimamizi wa mapato na na hivyo kuitaka menejimenti kushirikiana na Watendaji na Madiwani ili kuhakisha kuwa mapato yanakusanywa kwa weledi, ubunifu na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.
Wakiwasilisha Taarifa za Kata mbalimbali Madiwani wamepongeza jitihada kubwa inayofanywa na Serikali kupitia ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya vyumba vya madarasa na ujenzi wa vituo vya afya katika Kata ya Mjimwema,Luponde na Iwungilo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe