Februari 27,2024 Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Mhe. Deo Mwanyika akiongozana , Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe Thadei Luoga pamoja na watalamu wa Halmashauri wamapokea ugeni kutoka Ofisi ya Rais Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wakiambatana na wadau kutoka Benk ya Dunia (World Bank) .
Ugeni huo umefika Halmashauri ya Mji Njombe kwa lengo la kutembelea, kukagua na kuona hali halisi ya maandalizi kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya Miji ya Tanzania, Tanzania Cities Transforming Infrastructure and Competitiveness (TACTIC).
Katika ziara hiyo wametembelea maeneo mbalimbali ya uwekezaji yaliyotengwa na Halmashauri pamoja na kukagua barabara ambazo zinachangamoto kwa ajili ya kuziingiza katika mradi utakapoanza kutekelezwa.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe