Mafunzo kwa maafisa tarafa na watendaji wa kata mkoa wa Njombe yamemalizika kwa nasaha za utendaji kazi bora kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe Antony Mtaka.
Mkuu wa Mkoa Mtaka amezungumza na watumishi hao wakati akifunga mafunzo yaliyo andaliwa na Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa(TAMISEMI),Akiwataka Maafisa na Watendaji hao kwenda kuwajibika na kusimamia vema fedha za serikali kwakufuata sheria na miongozo mbalimbali ya serikali katika utendaji wao wa kazi.
"Miradi ya serikali ambayo ipo maeneo yenu tunaomba tukaone mabadiliko chanya kwasababu mafunzo yameshatolewa na tunategemea usimamizi mzuri katika katika miradi na ufuatiliaji katika maeneo yenu ili tuweze kupata matokeo mazuri ya serikali."
Akizungumza kwa niaba ya waliohudhuria mafunzo hayo Katibu tarafa ya Lupalilo Augustino Ngailo amesema wanamshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha mafunzo hayo kutolewa ili kwenda kuwasaidia kuboresha utendaji wa kazi za serikali kwa kiasi kikubwa hasa katika kuhakikisha serikali inapta mapato mengi na kwa usimamizi mzuri wa sheria za nchi.
''Kwa mafunzo ambayo tumeyapata tumekuwa wapya , tunakuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa tunakwenda kufanya kazi na sio kwa mazoea tena, hatutaiangusha serikali katika hili tunakwenda kufanya vizuri zaidi."
Kwa upande wake Mkurugenzi wa sera na mipango kutoka Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) John Cheyo amesema dhumuni la kuamua kufanya mafunzo hayo ni kutokana na changamoto nyingi za kiutendaji wanazokutana nazo watumishi zinazotokana na kukosekana kwa uelewa wa kina wa taratibu na miongozo ya utendaji kazi.
Mafunzo hayo yalifanyika kwa siku mbili(2) kuanzia Tarehe 7 Juni 2023 na kutamatika Tarehe 8,Juni 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe