Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Ayubu Mndeme amefungua mafunzo ya Mfumo mpya wa Ununuzi ujulikanao (NATIONAL e-PROCUREMENT SYSTEM OF TANZANIA) NeST kwa Mafisa Tehama ,ununuzi,na Wahandisi kutoka kwenye Halmashauri 6 za Mkoa wa Njombe.
Mafunzo hayo ya siku tano yamefunguliwa Septemba 4,2023 katika Ukumbi wa Halmashauri ya mji Njombe ambapo Kaimu Tawala Mkoa wa Njombe amesema mafunzo ya kujengewa uwezo wa matumizi ya mfumo huo mpya wa ununuzi (NeST) unaenda kurahisisha utendaji wa kazi za serikali katika ushindani kwa wazabuni ,uandaaji wa zabuni ndani ya mfumo na utaondoa matumizi ya karatasi (paper work) na Kila kitu kitafanyika ndani ya mfumo.
Akiendelea kuzungumza kaimu katibu tawala amesema ni muda sasa kwa wataalamu kuhakikisha mafunzo ambayo watayapata wanaenda kuyatumia vizuri ili kurahisisha utendaji wa kazi na kuwaomba kuzingatia taratibu zote ambazo zinatakiwa kuzingatiwa wakati wa ununuzi na kuwa tayari kuyatumia mafunzo ambayo yanatolewa.
Aidha Ndugu Ayubu Mndeme amezitaka taasisi zote kuhakikisha zienda kutumia mfumo huo mpya huku akiweka bayana kwa Taasisi au Halmashauri ambazo hazitatumia mfumo huu wa NeST mabadiliko ya sheria inatoa adhabu kwa Taasisi ya shilingi milioni 10,000,000/=
Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo kwa maafisa hao yameanza Septemba 04,2023 na yatafungwa Septemba 08,2023
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe