Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango leo Agosti 1,2022 mkoani Mbeya amefungua maonesho ya sherehe za Nane nane ambayo kitaifa yanafanyika katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya
Mhe.Dkt Mpango akiwa na Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe amekata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi maonesho hayo kwa mwaka huu 2022.Katika hotuba yake Mhe.Dkt Mpango amepongeza maandalizi mazuri yaliyofanyika na kuwapongeza wakulima, wafanyabiashara na taasisi mbalimbali kwa kushiriki katika maonesho hayo.
Aidha Mhe.Makamu wa Rais amesisitiza suala la kilimo biashara na kuwahakikisha wakulima upatikanaji wa pembejeo za kilimo na mbolea, "Serikali imejipanga kuhakikisha wakulima, wafugaji wanapata pembejeo za kilimo, mbolea kwa wakati na bila usumbufu" Alisema Mpango
Awali katika ufunguzi wa maonesho hayo Dkt. Mpango alitembelea katika mabanda mbalimbali na kujionea shughuli zinazofanywa na Wakulima,Wafugaji na Taasisi mbalimbali.Mfugaji wa samaki kutoka katika Kijiji cha Magoda Kata ya Uwemba Halmashauri ya Mji Njombe ni miongoni mwa wafugaji waliobahatika kutembelewa na Makamu wa Rais ambapo ameeleza kuwa sababu kubwa iliyomfanya kutumia teknolojia ya ufaugaji samaki kwa kutumia nyumba kitalu ni kutokana na hali ya hewa ya Njombe kuwa ya baridi na hivyo kupelekea samaki kutokuku kwa haraka lakini matumizi ya nyumba kitalu yamesaidia samaki kukua kwa haraka.
Makamu wa Rais ametoa rai kwa Taasisi za kifedha hapa nchini kuendeleza jitihada za kuweka masharti nafuu ya upatikanaji wa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi ili kuongeza uwekezaji na uzalishaji katika sekta hizo na kupunguza changamoto za ajira.
Kauli mbiu ya maonesho ya Nane Nane 2022 "Ajenda 10/30: Kilimo ni Biashara, Shiriki Kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe