• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Mapambano dhidi ya UKIMWI yawakutanisha wadau Njombe

Tarehe iliyowekwa: March 20th, 2020

Wadau wanaoshiriki katika mapambano dhidi ya UKIMWI katika Halmashauri ya Mji Njombe wamekutana kwa lengo la kujadili utekelezaji wa shughuli zinazofanywa kwenye mapambano na changamoto zinazowakabili.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau Mwenyekiti wa Kamati ya kudhibiti UKIMWI Halmashauri ya Mji Njombe Ester Mwageni ameyataka Mashirika binafsi kuendelea kupambana na Maambukizi kuanzia ngazi za shule ya msingi ambapo wanafunzi wengi wamekuwa hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na maambukizi huku akiisihi jamii kuendelea kuwalea watoto katika maadili.

“Tusiendelee kuzoea janga la UKIMWI. Elimu juu ya madhara ya VVU bado inahitajika kwa jamii kwa kiasi kikubwa. Wanafunzi wa Shule za Msingi wengi hawana elimu ya kutosha na wapo kwenye hatari kubwa” Alisema Mgeni

Mratibu wa UKIMWI Halmashauri ya Mji Njombe Daniel Mwasongwe  amesema kuwa Dira ya Mapambano hayo ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2030 ni kuwa na jamii isiyokuwa na maambukizi mapya ya VVU na kufikia 03 ambazo ni Maambukizi mapya kuwa 0,vifo vitokanavyo na VVU 0,unyanyapaa na ubaguzi wa WAVIU kuwa 0.

Kwa upande wao wawakilishi wa Mashirika yanayoshiriki katika mapambano hayo akiwemo Shedrack Mahenge Mratibu kutoka Shirika la SECO na Bariki Mhagama Mwezeshaji kutoka Shirika la COCODA wanasema kuwa licha ya kuwa jitihada zimekuwa zikifanyika kutoa elimu na kuwafikia wanufaika kwa njia mbalimbali bado changamoto kubwa imeendelea kuwa jamii hususani vijana kutokuwa na mwamko wa kutosha kushiriki katika semina na makongamano yanayohusu UKIMWI.

Aidha wameelezea kuwa kwa upande wa wadau wa mapambano hayo yapo Mashirika ambayo yamekuwa yakitoa taarifa ambazo sio sahihi kwa lengo la kujipatia fedha  kutoka kwa Wafadhili ambapo imepelekea Wanufaika wengine kuandikishwa zaidi ya mara moja na  kukosekana kwa taarifa sahihi za Mnufaika katika majalada pindi Mradi unapokuwa umeisha.

Maoni yaliyotolewa na Wadau hao ni pamoja na kuhakikisha kuwa Elimu inaendelea kutolewa kwa Wanafunzi na kuhakikisha kuwa katika vikao vya maendeleo ya Shule vya wazazi agenda ya VVU inajadiliwa ili wazazi nao waweze kufahamu jukumu walilonalo kwa watoto wao.

Kikao hicho kilihusisha wadau kutoka katika Mashirika ya COCODA, HHU, DREAM, AGAPE, SECO na NSHIDA ambao wote wapo katika mapambano hayo katika Halmashauri ya Mji Njombe

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe