Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa fedha zaidi ya shilingi Milioni 583 kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kujenga Shule Mpya ya Sekondari ya Amali katika Halmashauri ya Mji Njombe.
Shule hii mpya itajengwa katika kijiji cha Magoda kilichopo kata ya Uwemaba ambapo kukamilika kwake pamoja na kutoa masomo mengine itatoa mafunzo ya kiufundi katika nyanja mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia vijana kupata ujuzi wa moja kwa moja unaoweza kuwapatia ajira au uwezo wa kujiajiri.
Hii inatarajiwa kuwa suluhisho la changamoto kwa vijana kutegemea ajira mara baada yakumaliza masomo.
Ujenzi wa shule hii unatarajiwa kukamilika kufikia mwishoni mwa mwaka 2024 na kuanza kupokea wanafunzi rasmi mwanzoni mwa mwaka wa masomo wa 2025.
#kaziiendelee
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe