• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Mara baada ya kuziburuza Halmashauri za Miji kwenye mashindano ya usafi,Halmashauri ya Mji Njombe yaipiga msasa Manispaa ya Sumbawanga

Tarehe iliyowekwa: January 24th, 2019

Halmashauri ya Mji Njombe imepokea ugeni wa Waheshimiwa Madiwani wakiambatana na Wataalamu kutoka katika Manispaa ya Sumbawanga   lengo ikiwa ni kujifunza na kuongeza maarifa kuhusiana na maswala ya mapato na usafi wa Mazingira.

Haya yamebainika wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha wageni hao iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe, ambapo ugeni huo ulikiri wazi kuwa wamevutiwa kufika Halmashauri ya Mji Njombe kujifunza kutokana na sifa ambazo Halmashauri imekuwa ikijizolea kila mara katika eneo la usafi wa Mazingira pamoja na ukusanyaji mapato.

“Halmashauri ya Mji Sumbawanga kwa mwaka wa fedha 2017/2018 tulikasimia kukusanya bilioni mbili na milioni mia tano, lakini hatukufanikiwa kukusanya asilimia 80 kwa mujibu wa maagizo ya Mhe. Waziri Mkuu tulikusanya asilimia 54 pekee. Kwa upande wa mashindano ya usafi na Mazingira tulishika nafasi ya pili kutoka mwisho kutokana na ukosefu wa vyoo bora na matumizi bora ya vyoo.”Alisema Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mhe. Justin Emmanuel Malisawa.

Alifafanua kuwa changamoto kubwa ambayo imekuwa ikiwakabili ni kwenye utekelezaji wa sheria ndogo ndogo za Halmashauri na changamoto kutoka kwa wanasiasa ambao wamekuwa wakipinga na kutotekeleza ipasavyo baadhi ya maazimio waliyojiwekea kwenye ukusanyaji wa mapato na utunzaji Mazingira na ndio maana waliona umuhimu wa kuja kujifunza kutoka Njombe.

Akielezea mafanikio ya Halmashauri ya Mji Njombe ambayo imefikia kwa upande wa usafi wa Mazingira sambamba na ukusanyaji mapato, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe, Bi Illuminata Mwenda amesema kuwa mafanikio hayo yalitokana na utayari na kujitoa kwa Madiwani bila  kujali itikadi za vyama vyao na ushirikiano wa Wataalamu.

“Madiwani ndio wanaotaka Halmashauri yao iweje, hivyo ndivyo ninavyofahamu. Mnaweza mkawa na mipango mizuri lakini Waheshimiwa Madiwani wakisema hapana inakuwa ndivyo. Madiwani wetu agenda zao kuu ni mapato na usafi. Na hata katika vikao vya wataalamu tumekuwa tukijadili na kuboresha mapungufu yanayojitokeza na kuweka mikakati thabiti kwenye ukusanyaji mapato na usafi wa Mazingira na tumekuwa tukifanikiwa kwa kiasi kikubwa.”Alisema Mwenda.

Dorcas Mkello ni Mweka Hazina wa Halmashauri ya Mji Njombe ambaye yeye amesema kuwa miongoni mwa mbinu ambazo wamekuwa wakizitumia kwenye ukusanyaji mapato ni sambamba na utoaji wa motisha ya pikipiki kwa watendaji wanaofanya vizuri kwenye ukusanyaji mapato na kutoa milioni 5 kwa kila Diwani kwa kila robo ya mwaka fedha ambazo hukabidhiwa kwa diwani wa  Kata husika kwa ajili ya kuchochea maendeleo kwenye Kata yake. Hivyo kupitia fedha hizo, kila diwani amekuwa mlinzi kwenye usimamizi wa mapato kwani wasipofanya hivyo wanaelewa fika fedha hizo hazitapatikana bila kukusanywa kwa nguvu kubwa.

Afisa Mazingira Halmashauri ya Mji Njombe Lawi Bernard amesema kuwa licha ya kuwa na mwamko chanya wa wananchi kwenye uchangiaji wa tozo za taka, Halmashauri kupitia mapato ya ndani imekua ikiona umuhimu wa kuiwezesha idara hiyo na ndio maana kwa mwaka wa fedha 2018/2019 walifanikiwa kutenga fedha kupitia mapato ya ndani na kununua tractor kwa ajili ya kubeba taka na hivyo kuzuia mlundikano wa taka katika maeneo ya Mji kutokana na uwepo wa vitendea kazi vya kutosha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Edwin Mwanzinga alisema kuwa, siri ya mafanikio ni umoja baina ya Waheshimiwa Madiwani na wataalamu kwani wamekuwa wakipokea maelekezo ya wataalamu na panapokuwa na mapungufu wamekuwa wakishirikiana kuboresha kwa manufaa ya Halmashauri nzima.

“Wenzangu wa Sumbawanga niwaombe muwe na ushirikiano katika ukusanyaji mapato. Maendeleo ni ya wananchi wote na hayana vyama, naomba pia mfahamu kuwa katika swala la Usafi na Mazingira hamtaweza kufanya vizuri kwa kutegemea Halmashauri itaondoa taka yenyewe, lazima mzalisha taka awe na jukumu la kuondoa taka kwa kuchangia gharama.”Alisema Mwanzinga.

Aidha, Waheshimiwa Madiwani na Wataalamu kutoka Manispaa ya Sumbawanga wameishukuru Halmashauri ya Mji Njombe kwa elimu waliyoipata na wamepongeza ujenzi wa kiwango cha hali ya juu unaoendelea  katika kituo kipya cha Mabasi na wameahidi kutengeneza mtandao wa mawasiliano na Halmashauri ya Mji Njombe ili kuendelea kupata ujuzi na mbinu mpya katika maeneo mbalimbali.

Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Mji Njombe kwa miaka miwili mfululizo; 2017/2018 na 2018/2019 imepokea wageni kutoka Halmashauri nane za Mikoa ya Songwe, Singida, Shinyanga na Rukwa kwaajili ya kujifunza mbinu na siri ya ushindi inayotumia Halmashauri ya Mji   Njombe katika kuimarisha hali ya usafi katika maeneo yake yote.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe