Mkuu wa Wilaya Njombe Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa amepiga marufuku ununuzi wa parachichi daraja la Pili (reject) katika Wilaya ya Njombe unaofanyika bila uthibitisho wa kitaalamu na kibali kutoka Serikalini.
Mhe Kissa ametoa agizo hilo Juni 3,2024 alipokuwa akizungumza na wakulima wa parachichi wa Halmashauri ya Mji Njombe pamoja wanunuzi wa parachichi wiliopo katika wilaya ya Njombe.
"Hataruhusu mnunuzi yeyote wa Parachichi kununua parachichi daraja la pili (Reject) pasipo kibali kutoka serikalini.Kumekuwa na wanunuzi ambao wananunua parachichi daraja la pili kwa kujipangia bei wenyewe wakiwatisha wakulima kuwa zitaoza au zitawafia jambo ambalo linapelekea malalamiko kwa baadhi ya wakulima wa parachichi kuuza parachichi daraja la pili kwa bei ndogo ya shilingili 200”. Alisema Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa.
Aidha amewaagiza maafisa ushirika wote wa Wilaya ya Njombe kuhakikisha wanaanzisha ushirika wa umoja wa wakulima wa Parachichi (AMCOS) kutokana na mwongozo wa Wizara ya kilimo kubaini umhimu wa ushirika huo ambao utaimarisha mshikamano kwa wakulima na utasaidia wakulima wa Parachichi kuwa na lugha moja katika utendaji kazi.
Mkuu wa Wilaya Njombe pia amepiga marufuku uvunaji na ununuzi wa parachichi kwa kutumia mifuko (kiroba) jambo ambalo amesema linahatarisha ubora wa zao hilo katika soko la kimataifa huku akiyaomba makapuni ambayo yana lalamikiwa na wakulima katika ununuzi wa parachichi kwa bei ya chini kuacha tabia hiyo mara moja.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe