Wakala wa uuzaji wa mbolea Wilayani Njombe wametakiwa kuuza mbolea za ruzuku kwa kufuata bei elekezi iliyotolewa na serikali.
Kauli hiyo imetolewa Septemba 13,2023 na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe Kissa Gwakisa Kasongwa wakati akifunga kikao kilichowakutanisha mawakala wa kuuza mbolea,vyama vya ushirika vya wakulima,maafisa kilimo na viongozi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kanda ya nyanda za juu kusini ,kwa lengo la kufahamu maendeleo kwenye maandalizi ya uuzaji wa mbolea za ruzuku kuelekea msimu ujao wa kilimo wilayani njombe.
Amesema wauzaji wote wa mbolea wanapaswa kuzingatia bei iliyotolewa na serikali ili wasiwaumize wakulima wa Njombe ambao wanategemewa na taifa kwenye uzalishaji hasa wa mazao ya chakula.
“Mhe Rais wetu alielekeza bei elekezi zitolewe,na mimi kama mkuu wa wilaya naelekeza bei elekezi zifuatwe tusije tukaonana wabaya”
Aidha amezielekeza Halmashauri zote za wilaya ya njombe kuongeza muda wa usajili ili wakulima ambao hawakuandikishwa wasikose fursa.
“ Kama madftari yalishakuja huku yatafutiwe namna kuanzia kesho septemba 14 ,2023 madaftari yarudishwe saiti ,muda hautusubiri mvua hazitusubiri ,hili lifanyike mara moja wale wakulima ambao bado hawajaandikishwa wandikishwe na itafutwe namna nzuri yakuchukua yale madaftari ili kusajili majina kwenye mfumo”
Kuhusu vifaa vya kupia udongo ambavyo vipo kwenye kila Halmashauri amesema vyama vya ushirika vipewe kipaumbele cha kupima afya ya udongo ili waweze kutambua aina ya mbolea inayofaa kwenye ardhi wanayoitumia kwa shughuli za kilimo.
Katika hatua nyingine Mhe. Kissa Kasongwa ameelekeza bei elekezi za mbolea zibandikwe kwenye maeneo ya jumuiya na kwenye ofisi za serikali za kata na vijiji ili wananchi wote waweze kufahamu bei hizo,lengo ikiwa ni kuzuia udanganyifu kwenye bei.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe