Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji wa Njombe Bi Kuruthum Sadick amemwomba Mwenyekiti wa Mtaa wa Mji mwema kuanzisha tena upya mchakato wa kutatua mgogoro wa ardhi kati ya Familia ya Mligiliche na Shule ya Msingi Mji Mwema ili kuweza kuumaliza mapema mgogoro huo.
Ametoa agizo hilo Julai 23 ,2024 kwenye kikao kilichofanyika eneo la mgogoro kikijumuisha wataalamu na Wajumbe wa Mtaa wa Mji Mwema kwa lengo la kujadili undani ili kupata suluhu ya mgogoro huo uliodumu kwa muda wa miaka mitano (8) tangu mwaka 2017.
“Niombe Mwenyekiti na Mtendaji wa Mtaa nimesikiliza kwa urefu zaidi jambo hili , tuandae mchakato mpya ambao utatusaidia sisi kubaini ukweli wa jambo la yupi ni mmiliki wa ardhi na yupi sio Mmiliki halali, Serikali haipo kwa ajili ya kumuonea mtu na wala kumdhulumu mtu ,lengo letu kila moja apate haki sawa” Alisema Bi.Kuruthum Sadick ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe.
Mchakato wa kushughulikia mgogoro huo utatangazwa tena pale ambapo mlalamikaji ambaye ni familia ya Mligiliche itakapo kamilisha vielelezo vyote vya umiliki wa ardhi pamoja na wanafamilia hao na Shule ya Msingi Mji Mwema itakapo leta maelezo na nyaraka za umiliki wa kipande cha ardhi hicho ambacho kina lalamikiwa na wanafamilia hao.
Kikao cha Kutatua Mgogoro huo kilihudhuriwa na Afisa Mipango Mji ,Afisa Malalamiko ,Diwani wa Kata na Uongozi wa Mtaa wa Mji mwema pamoja na wajumbe wamtaa Mjimwema.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe