Timu ya wataalamu (CMT) kutoka Halmashauri ya Mji Njombe Septemba 30,2025 imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya shilingi 2,224,466,686.90.
Ziara hiyo imelenga kuangalia hatua za utekelezaji wa miradi hiyo na kujiridhisha kama fedha zilizotolewa zinatumika kwa usahihi, ufanisi na kwa kuzingatia thamani halisi ya fedha.
Aidha, timu hiyo ilitoa maelekezo kwa wakandarasi na wasimamizi wa miradi kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati, viwango vinazingatiwa na thamani ya fedha inaonekana moja kwa moja kupitia kazi zinazofanyika.
Timu hiyo ya wataalamu ilikagua miundombinu ya :-
Ujenzi wa shule mpya ya Elimu ya awali na msingi ya mkondo mmoja Mgola unaogharimu kiasi cha shilingi 329,500,000.00.
Ujenzi wa madarasa 2 na matundu 6 ya vyoo S/M Nazareti unaogharimu Tsh 70,100,000.00.
Ukarabati wa Shule ya Msingi Kambarage kwa gharama ya Tsh 132,830,905.00
Ujenzi wa madarasa 3 na matundu 6 ya vyoo S/M Kibena kwa gharama ya Tsh 88,000,000.00.
Ujenzi wa bweni S/S Anne Makinda kwa gharama ya shilingi 138,115,219.16
Ujenzi wa Zahanati kijiji cha Yakobi Tsh 131,653,194.29.
Ujenzi wa bweni shule ya sekondari Kifanya linalogharimu Tsh 138,115,219.16.
Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Kibena kwa gharama ya Tsh 900,000,000.00.
Ujenzi wa Zahanati katika Mtaa wa Kambarage inayogharimu Tsh 134,152,149.29 pamoja na ukamlishaji wa zahanati ya kijiji cha Itipula kwa gharama ya Tsh 162,000,000.00
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe