Mgogoro wa umiliki wa Ardhi uliodumu tangu miaka 1990 na kuendelea kwa muda mrefu kati ya familia ya Likiwilike katika kijiji cha Ihanga na Iboya Kata ya Ihanga, Halmashauri ya Mji Njombe, umetatuliwa mbele ya Katibu Tawala Wilaya ya Njombe Bi.Agatha Mhaiki katika kikao maalum kilichofanyika Tarehe 11 Februari 2025 katika eneo la mgogoro.
Katika kikao hicho, ambacho kilihusisha viongozi wa vijiji husika, maafisa wa ardhi, na wananchi wahusika katika mgogoro huo,ilibainika kuwa eneo hilo lina ekari 247 iliamuliwa kuwa Ofisi ya Mkurugenzi kupitia Ofisi ya Ardhi Halmashauri ya Mji Njombe ipime upya eneo hilo.
Baada ya upimaji huo, ekari 100 zigawiwe kwa mhusika wa mgogoro huo kama alivyoomba na kugawiwa mnamo mwaka 1990, na ekari zitakazobakia Serikali za vijiji vyote viwili zikae na kupanga namna ya kuzigawanya kwa matumizi mbalimbali na wananchi wengine waliomo katika maeneo hayo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe