Mgogoro wa ardhi kati ya familia ya Joseph Wella, aliyewahi kuwa mkazi wa Kijiji cha Liwengi Serikali ya kijiji hicho umepatiwa maamuzi Tarehe 11 Februari 2025 na Katibu Tawala wa Wilaya ya Njombe, Bi.Agatha Mhaiki, kwa kushirikiana na wataalam wa ardhi pamoja na Dawati la Malalamiko kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe.
Baada ya uchunguzi wa kina, imebainika kuwa familia ya Wella iliishi katika eneo hilo kabla ya operesheni Sogeza ambapo familia hiyo ilihamia Kijiji cha Kifanya. Mwaka 1974, baada ya kuanzishwa rasmi kwa Kijiji cha Liwengi, eneo hilo lilisalia chini ya mamlaka ya kijiji na likaendelezwa kwa kujengwa Ofisi ya Kijiji, ambayo inatumika hadi sasa.
Kwa kuzingatia sheria, kanuni, na taratibu za ardhi, Katibu Tawala wa Wilaya ameagiza kuwa eneo hilo litaendelea kuheshimiwa kwa matumizi ya umma. Aidha, ameielekeza familia ya Wella kuwasilisha maombi rasmi kwa uongozi wa kijiji ili yaweze kujadiliwa iwapo wanataka kurejea kijijini hapo,
Pia ameielekeza Serikali ya Kijiji cha Liwengi kushughulikia suala hili kwa kuangalia uwezekano wa kuwapatia familia ya Wella ardhi mbadala ili kutatua changamoto hiyo kwa haki na maridhiano.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe