Mgogoro wa Ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 15, uliohusisha mipaka na eneo la malisho kati ya kijiji cha Kisilo kilichopo kata ya Lugenge na kijiji cha Ihalula kilichopo kata ya Utalingolo , Julai 22, 2024 umetatuliwa baada ya wataalamu wa Halmashauri ya Mji Njombe kuonesha mipaka kwa mujibu wa ramani za upimaji kwa uongozi wa Kata za Lugenge na Utalingo na Serikali ya kijiji cha Kisilo na ihalula na kukubaliana mipaka hiyo iheshimiwe.
Katika eneo la malisho imeelekezwa wote waliovamia waondoe miti yao na eneo hilo libaki kwa ajili ya malisho.
Aidha viongozi wa pande zote mbili wamekubaliana kutumia machungio hayo kwa pamoja.( Communal land use).
Akitoa maelezo hayo Mtaalamu wa Mipango Miji na Kaimu Afisa Maendeleo ya Ardhi Mji wa Njombe Emmanuel Amos Luhamba ameeleza kuwa ni vizuri eneo hilo liheshimiwe na litumike kwa ajili ya machungio.
Kwa upande wake Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji Njombe Wakili Dotto Kulaba ameelekeza kuheshimu mipaka ya vijiji hivyo na eneo la malisho.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe